Dear
God by Kala Jeremiah
Intro:
Rock town records
Dear God let me to talk you
cause am in jungle God
I need your help
I watch my back
I see myself!!
Rock town records
Dear God let me to talk you
cause am in jungle God
I need your help
I watch my back
I see myself!!
Verse:
Asante Mungu leo ni siku nyingine
nakuja mbele yako baba nina ombi jingine
Baba wewe ndo kimbilio sina tena mwingine
si unacheki sina furaha kama watu wengine
Wengine wanakula bata na kusaza zingine
mimi bado niko ziro na masela wengine
Pengine labda umesisahau au umenichoka pengine
lakini hapana we sio kama viumbe wengine
Uliniumba wewe baba sio mtu mwingine
tena mimba yangu ililelewa na baba mwingine
Baba alikua busy na mademu wengine
nimeshamsamehe mwambie ana mtoto mwingine
Mwambie nampenda sana sina baba mwingine
mwisho wayote mlaze pema kama watu wengine
Tukiachana na hayo nina mambo mengine
baba mziki wangu ndio tatizo kubwa jingine
Nachana sana promo wanapewa wengine
wengine wanasema niende kwa mganga pengine
Lakini mi nimebatizwa kama wakristo wengine
naijua Biblia zaidi ya vitabu vingine
Lakini mi nimebatizwa kama wakristo wengine
naijua Biblia zaidi ya vitabu vingine
Mungu wa islael Mungu wa mataifa mengine
Mungu wa Yakobo Mungu wa Isaka Mungu watu wengine
Usikie kuomba kwangu unipe njia nyingine
Naombea watoto mayatima na wenye shida wengine
Wananchi maskini na tabaka jingine
Mungu baba tupe neema kama nchi zingine
Watembelee
mafisadi mmoja baada ya mwingine
wakumbushe
kula kwa jasho kama watu wengine
Ona
mpaka nasahau mengine
baba
ajira zipo chache hawapati wengine
Vijana
wanakula unga hawana kazi nyingine
dada
zetu wanajiuza wengine
Pengine
labda ndio sodoma na gomora nyingine
wanaume
sikuhizi ni mashoga wengine
Wanadai
haki zao kama haki zingine
wanaandamana
hadharani mataifa mengine
Wanaoana
kwa harusi kama ndoa zingine
tuachane
na hayo masuala nina swala jingine
Hivi ni
kweli umewatuma manabii wengine
maana
kila kukicha kuna kanisa jingine
Huyu
nabii na huyu ni nabii mwingine
huyu
anaponda na huyu anampinga mwingine
Wanahubiri
kuhusu pesa sio kitu kingine
toa
ndugu toa toa ulichonacho kingine
Mungu
nionyeshe njia nioneshe ishara nyingine
yapo
mambo mengi tu siwezi taja mengine
Hata
demu wangu nahisi ana mshikaji mwingine
mana
kabadilika kawa kama yule mwingine
Niliyemfuma
live akiwa na boya mwingine
nisamehe
dhambi ya kuzini sina dhambi nyingine
Mwokozi
wangu niongeze pesa zingine
rafiki
zangu niongeze tena wengine
Wawe
wote waukweli sio masnitch wengine
wakuchukua
siri na kuvujisha kwingine
Naombea
madaktari waongezwe posho zingine
ili
usije kutokea mgomo tena mwingine
Mana
walikufa watu wasije wakafa wengine
mwisho
wa yote nashukuru kwa uhai mwingine
Ninajua
sahizi watu wamelazwa wengine
rafiki
zangu walishagongwa na magari wengine
Kama Farook Warango na machizi wengine
mlaze pema Kanumba na rafiki wengine
Kama Farook Warango na machizi wengine
mlaze pema Kanumba na rafiki wengine
Tutaonana
Yesu akirudi kwa mara nyingine
asante
sana kwa baraza jingine
Japo
magamba yamevuka yakabaki mengine
classic
moja ina watu wengine
Wanadai
nchi imeuzwa kwa jamaa mwingine
Sajuki
Vengu na wagonjwa wengine
Wanyooshee
mkono wako wape Afya nyingine
Ameen!!
Ameen!!
No comments:
Post a Comment